Leopards kumteua tena Thomas Trucha kuwa kocha mpya

Dismas Otuke
1 Min Read

Klabu ya AFC Leopards inatarajiwa kumzindua Thomas Trucha raia wa Jamhuri ya Czech kuwa kocha mpya. 

Atamrithi Tom Juma aliyetimuliwa.

Trucha aliye na umri wa miaka 50, atakuwa anarejea kwa mara ya pili kuinoa Chui, baada ya kuwafunza kwa mwezi mmoja licha ya kutia saini mkataba wa miaka miwili mwaka 2020.

Trucha anatwaa mikoba ya ukufunzi kutoka kwa mchezaji nguli wa klabu hiyo Tom Juma aliyepigwa kalamu siku ya Jumatatu kutokana na msururu wa matokeo mabovu.

Ingwe inakalia nafasi ya 17 ligini kwa alama 3 pekee kutokana na mechi 6.

Share This Article