Waliokuwa mabingwa wa ligi kuu Uingereza Leicester City wamepandishwa ngazi kurejea kwenye ligi hiyo baada ya kuwa nje kwa msimu mmoja.
Leicester walipandishwa ngazi Ijumaa usiku baada ya watani wa jadi Leeds United kuambulia kichapo cha mabao 4 kwa nunge mikononi mwa Queens Park Rangers.
Leicester ambao watacheza mechi ya 45 April 29 dhidi ya Preston North End,wana pointi 94 ,alama nne zaidi ya Leeds United iliyo ya pili huku Ipswich ikikalia nafasi ya tatu kwa pointi 89.