Kuwa mke wa pili sio rahisi – asema Rita Edochie kuhusu Judy Austin

Marion Bosire
1 Min Read
Rita Edochie

Shangazi ya mwigizaji Yul Edochie Rita Edochie ambaye pia ni mwigizaji, amemtupia maneno mke wa pili wa Yul, Judy Austin.

Rita alitumia akaunti yake ya Instagram kupitisha ujumbe huo huku akijigamba kwamba anashukuru Mungu mume wake alimwoa yeye peke yake.

“Yaani hivi ndivyo ningekuwa napiga kelele kama mwehu alikwepa hospitali na kukimbilia sokoni? Siwezi.” aliandika mama huyo.

Usemi wake unafuatia hatua ya Judy Austin ya kuamua kuchapisha video ya kujibu wakosoaji wake mitandaoni, wengi waliodhania kwamba alianza uhusiano wa kimapenzi na Yul akiwa bado mke wa mtu.

Katika video yake Austin anasikika akipaaza sauti huku akisema ndoa yake ya kwanza ilivunjika, miaka kadhaa ikapita ndiposa akaja kukutana na Yul.

Yul Edochie, mke wake wa kwanza May na wa pili Judy wameangaziwa kwenye mitandao ya kijamii siku za hivi karibuni, kufuatia hotuba ya May kwenye mkutano wa kundi la wanawake.

May aliwaliza waliokuwa wakihudhuria mkutano huo pale aliposimulia jinsi ndoa yake iliingiliwa na Judy Austin ambaye Yul alitambulisha kama mke wake wa pili.

Rita anampendelea May kuliko Yul na amekuwa akionyesha wazi wazi kwamba hamuungi mkono Judy kuwa kwenye ndoa na Yul.

Website |  + posts
Share This Article