Kusudi la serikali ni kuboresha utoaji huduma kwa raia, asema Mudavadi

Martin Mwanje
1 Min Read

Serikali inapiga hatua madhubuti katika usimamizi wa utendakazi kwa lengo la kuboresha utoaji huduma.

Waziri Mwenye Mamlaka Makuu Musalia Mudavadi anasema shabaha ni kuchochea uwezo mkubwa uliopo katika sekta ya umma na kuhakikisha sekta hiyo inatiwa motisha ili kuongeza utoaji huduma kwa raia na kudumisha maslahi ya kitaifa.

Mudavadi aliyasema hayo alipokutana na Katibu katika Idara ya Masuala ya Bunge Aurelia Rono na Mwenyekiti wa Tume ya Mishahara Nchini, SRC Lyn Mengich afisi mwake leo Jumatano.

Mkurugenzi wa Shule ya Serikali Nchini Dkt. Ludeki Chweya ni mongoni mwa washikadau wakuu waliohudhuria mkutano huo wa ushauri kuhusu uboreshaji huduma katika utumishi wa umma.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *