KUPPET yashinikiza TSC kuharakisha nyongeza ya mishahara kwa walimu

Dismas Otuke
1 Min Read

Chama cha walimu wa shule za sekondari na vyuo nchini Kenya, KUPPET kimeitaka tume ya kuwaajiri walimu, TSC kuharakisha mchakato wa kuongeza mishahara ya walimu ili kuwakinga dhidi ya athari za matozo mapya.

Katibu Mkuu wa KUPPET Akelo Misori amelalamikia matozo mapya ya nyumba ambayo anasema yataathiri vibaya mishahara ya walimu kote nchini kutokana na kupanda kwa gharama ya maisha.

Mazungumzo baina ya TSC na vyama vya walimu vya KUPPET na KNUT yangali hayajakamilika, huku walimu wakilazimika kukatwa asilimia 3 ya mishahara mwishoni mwa mwezi Agosti kugharimia ushuru wa nyumba.

Haya yanajiri wakati ambapo makundi kadhaa yakiwemo cha mawakili nchini, LSK yamewasilisha kesi mahakamani kutaka utekelezwaji wa matozo mapya ya nyumba kusitishwa kwa misingi kuwa ni kinyume cha sheria.

TAGGED:
Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *