Chama cha Walimu wa shule za sekondari na vyuo KUPPET kimekataa kata kata ofa ya Waziri wa Elimu Julius Ogamba, kuwaajiri walimu wanagenzi kwa kandarasi ya kudumu kupitia usaili.
KUPPET wanahoji kuwa walimu hao tayari wamehudumu kwa zaidi ya miaka miwili, na wanapaswa kuajiriwa wote kwa kandarasi za kudumu na wala sio kwa awamu wala usaili.
Katibu Mkuu wa KUPPET Akelo Misori, ameitaka tume ya kuwaajiri walimu nchini TSC, kuwatendea haki walimu hao wanagenzi na kuwapa ajira ya kudumu kutokana na mchango wao mkubwa katika elimu ya Junior Secondary.
Akiwa mbele ya Bunge ,Waziri Ogamba alisema kuwa walimu hao wataajiriwa kwa awamu kupitia mahojiano ya ushindani.