KUJ yatoa ilani ya mgomo Standard Group

Marion Bosire
1 Min Read

Chama cha Wanahabari humu nchini – KUJ kimetoa ilani ya siku 14 ya mgomo kwa Waziri wa Leba Florence Bore kuhusu kile kilichokitaja kuwa ukiukaji wa haki za binadamu katika kampuni ya Standard Group.

Akizungumza katika kikao na wanahabari jana Jumapili jijini Nairobi, katibu mkuu wa KUJ Erick Oduor alisema kwamba wafanyakazi wa kampuni hiyo wamekosa kulipwa mishahara kwa muda wa miezi saba sasa.

Alikashifu suala hilo ikitizamiwa hali ngumu ya kiuchumi inayojiri nchini kwa sasa.

Oduor alilalamika pia kwamba wafanyakazi hao wako katika hatari ya kupoteza pesa nyingi ambazo wamewekeza kwenye chama chao ya akiba na mikopo kutokana na hatua ya mwajiri kukosa kuwasilisha makato yao.

Ameitaka kampuni ya Standard Group kubuni mpango mwafaka wa kulipa malimbikizi ya mishahara la sivyo wafanyakazi hao watalazimika kugoma.

Suala lingine alilozungumzia ni hatua ya kampuni hiyo ya kuweka kiwango kwa matumizi ya bima ya afya kwa wafanyakazi ambapo alitaka kiwango hicho kiondolewe.

Anataka pia usimamizi wa kampuni ukome kukusanya data ya wafanyakazi kama njia ya kuweka mfumo wa kufuatilia muda wao wa kuingia na kutoka kazini ilhali hawalipwi mishahara.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *