KUDHEIHA yamtaka Rais kuwanusuru wafanyakazi nusu milioni waliofurushwa kazini

Dismas Otuke
1 Min Read

Muungano wa wafanyikazi wa mikahawa, nyumbani na shuleni (KUDHEIHA) umemtaka Rais William Ruto kuingilia kati na kuwanusuru wafanyakazi zaidi ya nusu milioni waliokuwa wakifanya vibarua katika shule za sekondari nchini ambao tayari wamepokea barua za kusimamishwa kazi kuanzia tarehe mosi mwezi ujao.

Katibu Mkuu wa KUDHEIHA Albert Njeru amesema wahudumu hao ambao waliajiriwa kupitia kwa halmashauri ya shule na pia kwa mikataba wamearifiwa kutimuliwa baada ya serikali kuondoa mfumo wa shule za upili  kubadilisha na ule wa Sekondari ya Msingi, JSS.

Kwenye mfumo huo, wanafunzi wa JSS watasomea katika shule za msingi na wala sio shule za upili za awali.

Hali hii imewaacha wafanyakazi hao waliokuwa katika shule za sekondari bila ajira kuanzia mwaka ujao.

Njeru ameitaka Wizara ya Elimu badala yake kuwapa wafanyakazi hao majukumu mapya, badala ya kuwatimua na pia baadhi yao kupewa fursa ya kustaafu mapema na kupewa marupurupu.

Wafanyakazi walioathiriwa ni wale wanaofanya usafi, watengenezaji samani, wataalam wa maabara, wauguzi na makarani miongoni mwa wengine.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *