KUCCPS yalenga kuwasajili wanafunzi zaidi ya 12,000 kujiunga na TVET

Dismas Otuke
1 Min Read

Huduma mtandaoni ya kuwasajili wanafunzi kujiunga na vyuo nchini KUCCPS, inalenga kuwasajili wanafunzi Zaidi ya 12,000, kujiunga na vyuo vya kiufundi nchini maarufu kama TVET .

Kwenye taarifa kwa vyombo vya Habari KUCCPS imetanagza kupfungua Portal ikiwalenga wanafunzi 12,705 wanaotarajiwa kujiunga na mfumo wa masomo ya CBC, kuanzia Januari mwaka ujao.

Hii inafuatia agiozo la Waziri wa Elimu Ezekiel Machogu kuviutaka vyuo vyote vya kiufundi nchini kuanza kutekeleza ,fumo wa CBC.

Portal hiyo itafungwa rasmi Januari 4 mwaka ujao.

Kulingana na Afisa Mkuu Mtendaji wa KUCCPS Dkt Agnes Wahome ,wanafunzi watakaosajiliwa kujiunga na kozi za TVET watatahiniwa kwa kutumia mtaala wa CBC.

TAGGED:
Share This Article