KRG The Don atangaza kwamba anaacha muziki kwa muda

Marion Bosire
2 Min Read

Mwanamuziki wa mtindo wa Dancehall KRG The Don ametangaza kwamba anachukua pumziko kutoka kwa biashara ya burudani hususan uimbaji ili aangazie mambo mengine.

Kupitia mitandao ya kijamii, mwanamuziki huyo alielezea kwamba ana mambo mengi muhimu ya kushughulikia kama vile biashara zake ndiposa ameamua kupumzisha uanamuziki.

Aliandika, “Ninachukua pumziko refu kutoka biashara ya burudani. Ninataka kuelekeza nguvu zangu na muda kwa majukumu mengine na biashara ” akiongeza kwamba atapeza sana mashabiki wake lakini atakuwa humu humu.

Mwanamuziki huyo alielezea kwamba atarejelea muziki wakati atakuwa amewekeza shilingi bilioni moja kwenye akaunti ya benki akisema wanawe wanahitaji elimu bora na ni lazima awajibike.

KRG ambaye jina lake halisi ni Karuga Kimani hajakaa kwenye ulingo wa muziki kwa miaka mingi lakini kwa muda mchache ambao amedumu, amepata kujulikana sana hasa kutokana na mtindo wake wa maisha.

Alikuwa kwenye ndoa na Lina Wanjiru lakini walitengana na wanashirikiana katika malezi ya wanao watatu.

Huwa anajiita Bugaa na wakati fulani alisema thamani ya mali anayomiliki ilikuwa inakaribia shilingi bilioni tano na hivyo yeye ndiye mwanamuziki tajiri zaidi nchini Kenya.

Anamiliki kampuni ya usafiri kwa jina Taraja kati ya biashata nyingine nyingi ikiwemo sehemu ya burudani ya Casa Vera ambayo aliifunga mwezi wa pili mwaka huu wa 2024.

TAGGED:
Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *