Shirika la ndege la Kenya Airways, KQ limetangaza kurejeshwa kwa safari kati ya Nairobi-Maputo.
Safari hizo zilikuwa zimesitishwa kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita.
Hafla ya kutangazwa kurejeshwa kwa safari hizo ilifanyika leo Jumatano asubuhi katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta, JKIA.
Hafla hiyo ilihudhuria na Katibu katika Wizara ya Uchukuzi Mohamed Daghar, mwenzake katika Wizara ya Mambo ya Nje Korir Sing’oei, mwenyekiti wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga nchini Caleb Kositany, Balozi wa Msumbiji humu nchini Jeronimo Chivavi na Afisa Mtendaji wa KQ Allan Kilavuka.
“Hii ni hatua kubwa kuelekea kuimarisha uunganishaji wetu wa kikanda na kukuza ukuaji wa uchumi. Tumehongera kuona KQ ikipanua mawanda yake,” alisema Kositany wakati wa hafla hiyo.