KQ kurejelea safari zake za ndege kama kawaida Alhamisi

Martin Mwanje
1 Min Read

Shirika la ndege nchini la Kenya Airways, KQ leo Jumanne limetangaza kuwa litarejelea safari zake za ndege kama kawaida keshokutwa Alhamisi.

Hii ni baada ya safari hizo  kuvurugwa na hali mbaya ya hewa.

Kupitia taarifa kwa vyombo vya habari, KQ inasema inafanya kila iwezalo kurejesha hali ya kawaida katika ratiba ya safari za ndege ambayo ilivurugwa na hali mbaya ya hewa.

“Tungependa kuwashauri wageni wetu kwenye ratiba yetu inayotarajiwa ya safari za ndege juu ya mabadiliko yaliyosababishwa na hali mbaya ya hewa na kulazimu ndege kurejea kwenye uwanja wa ndege na ndege zetu tatu kufanyiwa ukarabati ambao haukuwa umepangwa,” ilisema taarifa kutoka kwa KQ.

Hata hivyo, shirika hilo linasema ndege zote zilirejeshwa ili kuanza tena kuhudumu kufikia Julai 3.

Limeongeza kuwa litawasiliana na wageni walioathiriwa kupitia ujumbe au baruapepe.

 

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *