Kampuni ya ndege nchini Kenya Airways, itarejelea safari za moja kwa moja kwa moja kutoka Nairobi hadi mjini Luanda,Angola kuanzia Machi mosi mwaka huu.
Haya yaliafikiwa siku ya Jumatano wiki hii kwenye kikao kati ya Rais William Ruto na mwe nzake wa Angola João Lourenço walipokutana jijini Accra,Ghana.
Angola pia inatarajiwa kuondoa masharti ya Viza kwa Wakenya wanaozuru nchini humo baada pia ya Kenya kuondoa hitaji hilo kwa raia wa Angola wanaozuru humu nchini.
KQ inatarajiwa kurejelea safari za moja kwa moja kutoka Nairobi hadi Luanda tarehe moja mwezi Machi,baada ya kuzisitisha mwaka 2020 wakati wa janga la Covid 19.