KQ: Hitilafu ya teknolojia duniani imeathiri utendakazi wetu

Martin Mwanje
1 Min Read

Shirika la ndege nchini la Kenya Airways, KQ linasema hitilafu ya teknolojia inayoshuhudiwa kote duniani imetatiza utendakazi wake. 

Hifilafu hiyo imeripotiwa kuathiri usafiri wa ndege kote duniani huku benki na mashirika ya utangazaji pia yakiripotiwa kutatizika.

Kwenye taarifa, KQ inasema mfumo wake wa kushika nafasi za usafiri umeathiriwa kutokana na hitilafu hiyo.

“Kwa sasa tunashuhudia hitilafu ya teknolojia ambayo imeathiri mfumo wetu wa kushika nafasi za usafiri kutokana na hitilafu ya teknolojia duniani. Wateja wanapaswa kutarajia huduma zinazotolewa kwa kasi ya polepole kuliko kawaida wakati tukitekeleza Mpango Wetu wa Undeleaji na Biashara,” ilisema KQ katika taarifa.

“Wateja wanaweza wakatembelea ofisi zetu za kushika nafasi ili kupata usaidizi. Tunaomba radhi kwa usumbufu wowote uliotokana na hali hiyo.”

Website |  + posts
Share This Article