Kampuni ya usambazaji umeme nchini (KPLC), imetoa ufadhili wa shilingi milioni 7.1, kwa makala ya mwaka huu ya mashindano ya WRC Safari Rally Kenya.
Ufadhili huo utajumuisha uwekaji taa za kutoa mwanga katika kituo cha Morendat kwa mashabiki na wanakijiji ili kufuatilia burudani ya mashindano hayo.
Kulingana na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya KPLC, Joseph Siror, watatoa umeme katika kituo cha kurekebisha magari cha Morendat.
Mashindano hayo yataanzishwa Alhamisi hii Rais William Ruto nje ya ukumbi wa Charter huku yakishirikisha madereva 48 kutoka nchi 18 tofauti.
KPLC pia itaweka kituo cha kuongeza umeme kwa magari ya umeme, pikipiki na simu za rununu.