Koskei: Kenya imejitolea kukabiliana na ufisadi

Tom Mathinji
1 Min Read
Mkuu wa utumishi wa umma Felix Koskei.

Mkuu wa utumishi wa umma, Felix Koskei, amesema kwamba, serikali imejitolea kikamilifu kukabiliana na ufisadi.

Koskei alisema kuwa uungwaji mkono wa kisiasa uliokuwa ukikosekana awali sasa upo, kutokana na msimamo mkali aliochukua rais dhidi ya ufisadi.

Koskei amesema kwamba, serikali tayari imweka huduma zake katika mitandao ya kidijitali, ili  kukabiliana na ufisadi katika taasisi za serikali.

Koskei ambaye alikutana na wakuu wa balozi mbalimbali za kigeni hapa nchini, alisema licha ya tume ya maadili na kukabiliana na ufisadi EACC, kujizatiti kukabiliana na ufisadi, ni vyema tume hiyo pia kuelekeza juhudi hizo pia kwa maafisa wa umma.

Katika mkutano huo, Koskei pamoja na mabalozi hao walikubaliana kwamba, ni vyema kutambua taasisi zilizoathirika pakubwa na ufisadi ili kuweza kuweka mikakati ya kukabiliana na jinamizi hilo.

Koskei aliwashukuru wakuu hao kwa kuendelea kutoa msaada wa kifedha katika kuimarisha taasisi za serikali ambazo ni muhimu katika kukabiliana na ufisadi kama vile EACC, idara ya DCI na ile ya DPP.

TAGGED:
Share This Article