Kosgei atwaa ubingwa wa Tokyo Marathon

Dismas Otuke
1 Min Read

Mshikilizi wa zamani wa rekodi ya dunia Brigid Kosgei, ametwaa ubingwa wa mbio za Tokyo Marathon huku akiweka rekodi mpya mapema Jumapili nchini Japan.

Kosgei alimeziparakasa mbio hizo kwa saa 2, dakika 14 na sekunde 29, muda wake wa pili wa kasi na muda wa saba bora duniani.

Bertikan Welde kutoka Ethiopia amemaliza wa pili kwa muda wa saa 2 dakika 16 na sekunde 36, huku mwenzake Haywi Feysa akifunga tatu bora kwa saa 2 dakika 17 na sekunde 39.

Geofrey Toroitich wa Kenya alimaliza wa pili kwa kutumia saa 2, dakika 3 na sekunde 37, muda sawa na mshindi Tade Tekele wa Ethiopia, sekunde moja mbele ya Alexander Munyao wa Kenya, aliyeridhia nafasi ya tatu.

Share This Article