Serikali ya Korea Kusini imelazimika kuondoa sheria za kijeshi ilizokuwa imewawekea raia wake, baada ya Wabunge kuwasilisha hoja ya kumbandua afisini Rais Yun Sook Yeol .
Wabunge wameanza mchakato wa kumtimua Rais Yeol, hali inayohatarisha uthabiti wa taifa hilo ambalo ni la nne kwa ukubwa kiuchumi barani Asia.
Ili kumbandua Rais, bunge linahitaji kupata thuluthi mbili ya kura za Wabunge watakaounga mkono hoja hiyo.
Huenda Rais huyo akafurushwa kwani chama cha upinzani cha Democratic na vyama vingine vidogo vina idadi ya Wabunge 199,vikikosa kura moja tu kufikisha kura 200 za kupitisha hoja hiyo.
Raia wamejitokeza barabarani nchini Korea Kusini mapema leo kuandamana kupinga hatua ya serikali kuweka sheria za kijeshi.