Kamishnaa Mkuu wa Polisi Japheth Koome alikutana na wajumbe wa usalama kutoka taifa la Haiti siku ya Jumatano katika afisi yake katika kaunti ya Nairobi.
Wajumbe hao wakiongozwa na kamishnaa mkuu wa polisi wa Haiti Frantz Elbe, walio nchini kufuatilia mpangilio wa serikali ya Kenya kutuma maafisa wa usalama 1,000 katika kisiwa hicho.
Tayari Bunge la Kenya limeidhinisha mchakato wa serikali ya Kenya kutuma polisi kushika doria nchini Haiti.