Kongamano la Walaji Duniani 2023 kuandaliwa Nairobi

Martin Mwanje
1 Min Read

Kongamano la Kimataifa la Walaji Duniani 2023 litaandaliwa jijini Nairobi kuanzia kesho Jumatano. 

Kauli mbiu ya kongamano hilo la siku mbili ni “Kujenga mustakabali thabiti kwa ajili ya walaji”.

Naibu Rais Rigathi Gachagua atalifungua kongamano hilo litakalowaleta pamoja washiriki kutoka nchi mbalimbali, kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa Mamlaka ya Ushindani Nchini Kenya, CAK.

Mawaziri wa Fedha Prof. Njuguna Ndung’u wa Kenya na Teshale Kefene Ethiopia ni miongoni watakaohudhuria.

Washiriki kutoka Tume ya Ushindani ya Soko la Pamoja la Mashariki na Kusini mwa Afrika, COMESA pia watahudhuria.

Kongamano hilo litaleta pamoja mavuguvugu ya walaji walio na ushawishi katika nyanya ya biashara, mashirika ya kijamii na wanazuoni kuangazia masuala yanayoikumba dunia na kuwalinda walaji kote duniani.

Hususan, wadau wa masoko watakuja pamoja kwa lengo la kuelewa tajiriba za walaji ndani na nje ya majanga na kujenga mustakabali thabiti kwa ajili ya watu na dunia.

 

 

Website |  + posts
Share This Article