Kombe la Dunia kwa wanawake: Mfungaji bora kubainika baada ya mechi mbili za mwisho

Dismas Otuke
1 Min Read

Kinyangányiro cha mfungaji bora kweny fainali za Kombe la Dunia mwaka huu nchini Australia na Newzealand kitabainika Jumapili hii, Agosti 20 wakati wa fainali kati ya Uhispania na Uingereza .

Mechi 62 zimechezwa kwenye kipute hicho na mabao 161 kufungwa.

Hinata Miyazawa wa Japani angali kuongoza chati ya upachikaji magoli akiwa na mabao matano akifuatwa na beki Amanda Ilestedt wa Uswidi aliyetikisa nyavu mara nne huku wanandinga wengine watatu wakiwa na magoli manne, nao ni Kadidiatou Diani wa Ufaransa, Alexandra Popp wa Ujerumani na Jill Roord wa Uholanzi.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *