Kipute cha Kombe la Dunia kwa wanawake kinang’oa nanga Alhamisi, Julai 20 nchini Australia na Newzealand, huku mataifa 32 yakishiriki kwa mara ya kwanza kutoka timu 24 zilizoshiriki mwaka 2019.
Afrika itawakilishwa na timu nne za Morocco na Zambia wanaoshiriki kwa mara ya kwanza.
Timu zingine ni Afrika Kusini na Nigeria.
Marekani italenga kunyakua kombe la tatu mtawalia baada ya kutawazwa mabingwa mwaka 2015 na 2019.
Kwa mara ya kwanza, FIFA imetangaza kuwalipa wachezaji moja kwa moja ambapo kila mchezaji atalipwa dola 30,000 na takriban dola elfu 70 kwa kila mchezaji kwa mabingwa wa makala ya mwaka huu.
Norway watacheza mechi ya ufunguzi ya kundi A dhidi ya wenyeji Newzealand kuanzia saa nne asubuhi kwa muda wa Afrika ya Mashariki.
Baadaye saa saba adhuhuri, wenyeji wenza Australia watavaana na Ireland katika kundi B.
Fainali ya mashindano hayo itasakatwa Agosti 20 huku tayari kwa mara ya kwanza katika historia, tiketi zaidi ya milioni moja zikiwa zimeuzwa.