Kombe la Carabao: Tottenham kumenyana na Man U

Dismas Otuke
1 Min Read

Tottenham Hotspur itawaalika Manchester United katika robo fainali kuwania kombe la EFL Carabao, baada ya vijana hao wa London kuwatema nje Manchester City mabao 2-1 jana usiku.

Man U nao walitinga raundi ya nane bora baada ya kuwachachafya Leicester City mabaoa 5-2 ugani Old Traford Jumatano usiku.

Katika droo hiyo ya kwota fainali katikati ya Disemba, Arsenal iliyowakwatua Preston magoli matatu bila jawabu imepangwa dhidi ya Crystal Palace iliyowalemea Aston Villa 3-1.

Newcastle United baada ya kuizabua Chelsea mabao 2-1 jana watachuana na Brentford iliyowalemea Shefield kupitia mikwaju ya penalti wakati Liverpool ikichuana a Southampton.

Liverpool iliwashinda Brighton mabao 3-2 huku Southampton ikiwakwatua Stoke City 3-2.

Share This Article