Kocha wa timu ya taifa ya Nigeria maarufu kama Super Eagles Jose Peseiro amehiaria kuondoka baada ya kuwasaidi kucheza hadi fainali ya kombe la AFCON makala ya mwaka huu nchini Ivory Coast.
Licha ya kushindwa kwenye fainali ya AFCON na wenyeji Ivory Coast kocha huyo wa kutoka Ureno aliye na umri wa miaka 63 ameamua kujiuzulu.
Peseiro amekuwa usukukani kwa miezi 12 na amejiuzulu kupitia kwa ujumbe alioandika katika mitandao yake ya kijamii.