Tume ya Kitaifa ya Kutetea Haki za Binadamu Nchini Kenya, KNCHR imetoa wito kwa wananchi kuendelea kutoa uhamasisho pamoja na mikakati ya kulinda na kuzuia matatizo ya akili.
Wito huou najiri huku taifa hilo likiungana na ulimwengu kuadhimisha siku ya kimataifa ya afya ya akili mwaka 2023, kauli mbiu ikiwa “Afya ya akili ni haki ya kibinadamu”.
Kupitia kwa taarifa, KCHR ilitoa wito kwa hospitali za afya ya kiakili kubuni mazingira bora ya utoaji huduma kwa waathiriwa wa matatizo ya kiakili, kama vile kusitisha hatua ya kuwafungia na kuwatibu wagonjwa bila hiari yao na kukiuka haki zao kupitia ghasia.
Aidha tume hiyo imetoa wito wa kuachiliwa kwa watu walio na matatizo ya akili wanaozuiliwa na taasisi za afya, familia au mashirika ya kidini.
Tume hiyo imehimiza serikali ya kitaifa na zile za kaunti kuongeza bajeti ya kushughulikia afya ya akili ili kuimarisha mifumo na upatikanaji wa huduma za afya ya akili katika jamii.