Kizaazaa cha Ligi Kuu ya Kenya kusitishwa kwa shamrashamra za Krismasi na Mwaka Mpya Jumapili hii

Dismas Otuke
1 Min Read

Ligi Kuu ya Kenya inatarajiwa kuchukua mapumziko ya sherehe za Krismasi na Mwaka Mpya, baada ya mechi za raundi ya 15 mwishoni mwa juma hili.

Mechi za Ligi  hiyo zinatarajiwa kurejea tarehe 4 mwezi ujao.

Katika mechi za mwishoni mwa juma hili, Bidco United watakuwa nyumbani dhidi ya Sofapaka hapo kesho kuanzia saa saba adhuhuri wakati Posta Rangera ikiwatumbuiza Sofapaka.

Baadaye mida ya saa tisa Kenya Commercial Bank watakuwa nyumbani dhidi ya Mara Sugar, Police FC wamenyane na Kakamega Homeboyz katika mchuano mwingine.

Jumapili, Talanta FC watakabiliana Muranga Seal, Ulinzi Stars ichuane na Nairobi City Stars wakati Bandari FC wakiwa nyumbani dhidi ya AFC Leopards kisha mashemeji Gor Mahia wahitimishe ratiba dhidi ya Kariobangi Sharks.

KCB na Tusker FC wangali kuongoza jedwali la ligi kwa alama 24 kila moja, wakifuatwa unyounyo na Police na  Bandari FC  katika nafasiza 3 na 4 kwa alama 23 na 22 mtawalia wakati mabingwa watetezi Gor wakifunga ukurasa wa tano bora kwa pointi 21.

 

TAGGED:
Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *