Kiungo wa zamani wa Harambee Stars Gatuso Okoth akamatwa kwa ubakaji

Dismas Otuke
1 Min Read

Kiungo wa zamani wa klabu ya Goar Mahia na timu ya taifa ya Harambee Stars Collins Gatuso Okoth, amekamatwa Jumatatu jioni na maafisa wa polisi kwa madai ya ubakaji na mauaji ya mtoto.

Okoth amepelekwa katika kituo cha polisi cha Pangani kwa uchunguzi .

Kisa hicho kiliripotiwa katika kituo cha polisi cha Lucky Summer tarehe 22 mwezi huu.

Yamkini Okoth ndiye mshukiwa mkuu kwenye mauaji ya msichana huyo menye umri wa miaka mitatu, ambaye mwili wake ulipatikana nyuma ya jengo moja ukiwa na majiraha shingoni, huku polisi wakishuku kuwa mwili huo ulitupwa hapo baada ya kuawa.

Mchezaji huyo atazuiliwa katika korokoroni kwa siku 21 na kufanyiwa utathmini akili katika hospitali ya Mathare ,kabla ya kufunguliwa mashtaka.

Website |  + posts
Share This Article