Kitita cha pesa kwa timu zinazoshiriki kipute cha AFCON

Dismas Otuke
1 Min Read

Mabingwa wa kombe la AFCON mwaka huu nchini Ivory Coast watatia kibindoni shilingi bilioni 1.12 huku washindi wa medali ya fedha wakipokea shilingi milioni 645. Timu mbili zitakazoshindwa katika hatua ya nusu fainali zitatuzwa shilingi milioni 403 kila moja.

Timu nne zitakazobanduliwa katika robo fainali zitawazawadiwa shilingi milioni 209 kila moja.

Mataifa mawili yaliyomaliza katika nafasi za tatu na kukosa kufuzu kwa hatua ya mwondoano yatapokea shilingi milioni 112 kila moja.

Timu sita zilizomaliza katika nafasi za nne katika makundi yote zitatia mkobani shilingi milioni 80 kila moja.

Share This Article