Kocha mkuu wa timu ya Kenya iliyomaliza ya pili kwenye mashindano ya Riadha Duniani mwezi jana mjini Tokyo, Japan, Julius Kirwa ndiye kocha bora wa mwezi Septemba katika tuzo za kila mwezi za chama cha Wanahabari za michezo nchini SJAK kwa ushirikiano na kampuni ya kamari ya Betika.
Kirwa aliongoza timu ya Kenya kumaliza ya pili katika mashindano ya riadha Duniani mjini Tokyo.
Kocha huyo amewashinda kocha wa timu ya mpira wa kikapu Nairobi City Thunder Bradley Ibs, kocha wa klabu ya raga ya KCB Andrew Amonde na kocha wa timu ya Kenya ya voliboli ya wanaume chini ya umri wa miaka 20 Luke Makuto.