Mabingwa wa Olimpiki Faith Kipyegon, Beatrice Chebet na Emmanuel Wanyonyina mshindi wa nishani ya shaba ya Olimpiki, Faith Cherotich,walitawazwa mabingwa wa Diamond League mwaka huu, katika sikubya pili na ya mwisho ya mkondo wa Memorial Van Damme Diamond League mjini Brussels, Ubelgiji jana usiku.
Cherotich ambaye pia ni mshindi nishank ya shaba ya dunia alishinda mbio za mita 3,000 kuruka viunzi na maji akiweka rekodi mpya ya mashindano hayo kwa kutumia dakika 9 sekunde 2.36, akimlemea bingwa wa Olimpiki Winfred Yavi wa Bahrain aliyemaliza w apili.
Mganda Peruth Chemutai aliridhia nafasi tatu.
Faith Kipyegon alinyakua taji ya tano ya Diamond League katika mita 1,500 akiongoza kutoka mita 300 za mwisho na kushinda akiweka rekodi mpya ya dakika 3 sekunde 54.75.
Diribe Welteji wa Ethiopia na Jessica Hull wa Australia walimaliza katika nafasi za pili na tatu mtawalia.
Bingwa mara mbili wa Olimpiki Beatrice Chebet alihitimisha msimu wake wa kufana kwa kushinda mita 5,000 kwa rekodi mpya ya dakika 14 sekunde 9.82.
Bingwa wa Olimpiki Emanuel Wanyonyi alitoka nyuma katika mita 50 za mwisho na kushinda mita 800 kwa dakika 1 sekunde 42.70,akifuatwa na Djamel Sedjati wa Algieria na Marco Arop wa Canada katika nafasi ya tatu.
Wanyonyi,Cherotich,Kipyegon,Chebet,Serem na Mary Moraa walijiunga na washindi wengine 26 waliotawazwa mabingwa.