Kipyegon,Chebet na Wanyonyi kuwania tuzo ya mwanariadha bora mwaka huu

Dismas Otuke
1 Min Read

Bingwa mara tatu wa Olimpiki katika mita 1500 Faith Kipyegon,Beatrice Chebet,na bingwa wa Olimpiki katika mbio za 800 Emmanuel Wanyonyi wameteuliwa kuwania tuzo za mwanariadha bora wa mwaka katika mbio za uwanjani kwa wanawake wanaume mtawalia kwenye tuzo zitakazoandiwa mjini Monaco,Ufaransa.

Kipyegon, Alieshinda tuzo hiyo mwaka jana ameteuliwa baada ya kusajili matokeo bora msimu huu alipovunja rekodi ya dunia mita 1500, akahifadhi taji ya Olimpiki, akashinda medali ya fedha katika mita 5,000 na na kutwaa taji ya Diamond League.

Chebet pia ametamba msimu huu alikuvunja rekodi ya dunia ya mita 10,000, kabla ya kushinda dhahabu za Olimpiki katika mita 5,000 na 10,000 jijini Paris, Ufaransa.

Wawili hao watapambana na mabingwa wengine wa Olimpiki wakwiemo: Julien Alfred wa Saint Lucia, Sydney McLaughlin-Levrone wa Marekani, Marileidy Paulino wa Jamhuri ya Dominica na, Gabby Thomas wa Marekani.

Emmanuel Wanyonyi atakabiliwa na upinzani mkali katika tuzo ya wanaume dhidi ya Wamarekani Grant Holloway na Noah Lyles, Jacob Ingebrigtsen kutoka Norway, and Letsile Tebogo wa Botswana.

Upigaji kwa mwanariadha bora wa kiume na wa kike unaendelea kupitia mitandao ya kijamii ya Shirikisho la riadha ulimwenguni na utafungwa usiku wa manane Oktoba 27 mwaka huu.

Share This Article