Bingwa wa dunia katika mita 5,000 Faith Kipyegon amewaongoza wenzake Margaret Chelimo na Beatrice Chebet, kufuzu kwa fainali ya mbio hizo baada ya kutamba katika mchujo wa Ijumaa.
Kipyegon ambaye ni bingwa mara mbili wa Olimpiki katika mita 1500 amedhibiti mchujo wa kwanza na kuongoza kwa dakika 14 sekunde 57.56, akifuatwa na bingwa mtetezi Sifan Hassan wa Uholanzi.
Margaret Chelimo Kipkemboi wa kenya pia amejikatia tiketi kwa fainali ya Jumatatu usiku baada ya kumaliza wa nne kwa dakika 14 sekunde 57.70.
Chebet ambaye ni mshikilizi wa rekodi ya dunia ya mita 10,000 ameongoza mchujo wa pili akizikamilisha kwa dakika 15 nukta 73.
Fainali ya shindano hilo itaandaliwa Jumatatu usiku.