Kipyegon na Kiptum kubaini mbivu na mbichi katika tuzo za mwanariadha bora wa mwaka

Dismas Otuke
1 Min Read
Faith Kipyegon

Bingwa mara mbili wa Olimpiki katika mita 1500 Faith Kipyegon, na mshikilizi wa rekodi ya dunia katika marathon ya wanaume Kelvin Kiptum wanawania tuzo ya mwanariadha bora wa mwaka huu.

Halfa ya mwaka huu itaandaliwa Jumatatu usiku mjini Monaco Ufaransa .

Kipyegon alivunja rekodi tatu ya mita 1,500,mita 5,000 na ile maili moja kando na kuhifadhi taji ya dunia ya mita 1,500 na pia akanyakua taji ya dunia katika 5,000.

Kiptum alivunja rekodi ya dunia iliyokuwa imishikiliwa na Eliud Kipchoge kando na kushinda mbio za London na Chicago akiweka rekodi mpya ya saa 2 na sekunde 35.

Share This Article