Kipyegon kuwaongoza Wakenya Ijumaa Mjini Rome,mashindano ya Diamond League

Dismas Otuke
1 Min Read

Bingwa mara tatu wa Olimpiki  katika mita 1,500 Faith Kipyegon atawaongoza Wakenya  katika mkondo wa 13 wa mashindano ya Diamond League ya Rome Italia Ijumaa usiku.

Kipyegon atashiriki fainali hiyo pamoja na Nelly Jepchirchir.

Mshindi wa nishani ya shaba ya Olimpiki Faith Cherotich atashiriki mita 3,000 kuruka viunzi na maji akipambana na bingwa wa Olimpiki Winfred Yavi kutoka Bahrain.

Mshini wa nishani ya fedha ya Olimpiki Ronald Kwemoi atashiriki mita 5,000 pamoja na Jacob Krop na Nicholas Kimeli.

Katika mita 100 Ferdinand Omanyala atashindana na bingwa wa Olimpiki katika mita 200 Letsile Tebogo wa Botswana ,Wamerekani Fred Kerley na Christian Coleman na Lamont Marcel Jacobs wa Italia.

 

Share This Article