Kipyegon kuwania taji ya tatu ya dunia mjini Budapest Hungary

Dismas Otuke
1 Min Read

Bingwa mara mbili  wa dunia katika mbio za mita 1500 Faith Kipyegon atalenga kunyakua dhahabu ya tatu ya shindano hilo atakapojitosa uwanjani katika raundi ya kwanza ya shindano hilo kuanzia saa tisa na robo.

Kipyegon aliye na umri wa miaka 29 baadaye pia atatimka mita 5000 huku akishikilia rekodi ya dunia .

Bingwa huyo mara mbili wa Olimpiki wa mita 1500 anajivunia kuwa na msimu bora mwaka huu akivunja rekodi tatu za dunia ndani ya kipindi cha miezi miwili,ile ya mita 5000,mita 1500 na maili moja.

Kipyegon alinyakua dhahabu za dunia katika mbio za chipukizi,mbio za nyika duniani mara mbili kabla ya kuanza kushiriki mbio za watu wazima.

 

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *