Bingwa mara mbili wa Olimpiki Faith Kipyegon amevunja Rekodi ya Dunia ya mita 1,500 katika mashindano ya Paris Diamond League Jumapili jioni.
Kipyegon ameweka rekodi mpya ya dakika 3 sekunde 49.04, akivunja rekodi yake mwenyewe ya Juni 2 mwaka uliopita ya dakiKa 3 sekunde 49.11.
Bingwa huyo mara mbili wa dunia alikuwa amekimbia muda wa kasi wa dakika 3, sekunde 53.98 wakati wa uteuzi wa Olimpiki uwanjani Nyayo mwezi uliopita.