Kipyegon ateuliwa kwa tuzo za Laureus

Dismas Otuke
1 Min Read

Bingwa mara mbili wa Olimpiki katik ambio za mita 1500 Faith Kipyegon, ameteuliwa kuwania tuzo ya mwanariadha bora wa kike wa mwaka huu katika tuzo za Laureus makala ya 25, yatakayoandaliwa mjini Madrid Uhispania Aprili 22.

Kipyegon ambaye pia ni bningwa mara tatu wa dunia katika mita 1500 ni miongoni mwa wanaspoti sita walioteuliwa kuwania tuzo hiyo, baada ya kushinda dhahabu mbili za dunia mwaka jana katika mbio za mita 1500 na 5,000 mjini Budapest,Hungary.

Mwanariadha huyo pia alivunja rekodi tatu za dunia ndani ya mwezi mmoja.

Kipyegon ameteuliwa pamoja na mabingwa wa dunia Sha’Carri Richardson wa Marekani,Shericka Jackson wa Jamaica, bingwa wa French Open Iga Świątek kutoka Poland, mshindi wa kombe la dunia Aitana Bonmatí wa Uhispania,na mtelezaji juu ya barafu Mikaela Shiffrin wa Marekani.

Kipyegon ambaye ni binga mtetezi wa Olimpiki pia atuzwa mwanariadha bora wa mwaka ,mwaka uliopita kwa wanariadha wa mbio za uwanjani.

Website |  + posts
Share This Article