Kipyegon apokea shahada ya uzamifu kutoka chuo kikuu cha Eldoret

Dismas Otuke
1 Min Read

Bingwa mara tatu wa Olimpiki katika mbio za mita 1,500 Faith Kipyegon,alikabidhiwa shahada ya uzamifu kutoka chuo kikuu cha Eldoret jana.

Kipyegon ambaye pia ni mshikilizi wa rekodi dunia katika shindano hilo, ndiye mwanariadha wa kwanza wa kike humu nchini kupokea shahada hiyo ya chuo kikuu cha Eldoret.

Kipyegon aliye na umri wa miaka 30 alipokea shahada hiyo kutokana na mchango wake kupitia miradi ya kijamii hususan wasichana.

Share This Article