Bingwa mara tatu wa Olimpiki klatika mbio za mita 1,500 Faith Kipyegon, alionyesha makeke yake kwa kutwaa ubingwa katika mkondo wa 13 wa mashindano ya Diamond league Ijumaa usiku mjini Rome,Italia.
Kipyegon ambaye pia ni bingwa mara mbuili wa Dunia aliziparakasa kwa dakika 3 sekunde 52.89.
Freweyni Hailu wa Ethiopia alimaliza wa pili kwa dakika 3 sekunde 54.16, huku mwenzake Birke Haylom akiridhia nafasi ya tatu.
Nelly Chepchirchir wa Kenya alimaliza wa tano.
Mshindi wa nishani ya shaba ya Olimpiki Faith Cherotich alimaliza wa tatu katika mita 3000 kuruka viunzi na Maji, akitumia muda wa dakika 8 sekunde 57.65.
Yavi Mutile wa Bahrain alishinda kwa dakika 8 sekunde 44.39, akikosea nukta 07 avunje rekodi ya Dunia ya Beatrice Chepkoech, wakati Mganda Peruth Chemutai akimaliza wa pili.
Jacob Krop na Nicholas Kimeli wa Kenya walimaliza katika nafasi za 4 na 9 mtawalia kwenye fainali ya mita 5,000.
Hagos Gebrehiwet,Yomif Kejelcha na Selemon Barega wote kutoka Ethiopia walifagia nafasi tatu za kwanza katika usanjari huo.
Bingwa wa Olimpiki katika mita 200 Letsile Tebogo wa Botswana alishinda fainali ya mita 100, akifyatuka kwa sekunde 9.87,akifuatwa na Christian Coleman na Fred Kerley wa Marekani katika nafasi za pili na tatu mtawalia.
Ferdinand Omanyala wa Kenya alimaliza wa 8 kwa sekunde 10.08 .