Kipute cha AFCON U 23 kuanza kutifua vumbi Jumamosi nchini Morocco

Dismas Otuke
1 Min Read

Makala ya tatu ya muchuano ya kuwania kombe la Afrika kwa chipukizi walio chini ya umri wa miaka 23, yataanza rasmi Jumamosi kwa mechi baina ya wenyeji Morocco dhidi ya Guinea ugani Prince Mouley Abdelllah jijini Rabat kuanzia saa tano usiku.

Pambaono la pili kundini A, litasakatwa Jumapili kuanzia saa kumi Alasiri, kati ya Ghana na Congo.

Katika mechi za kundi B siku ya Jumapili mabingwa watetezi Misri, watamenyana na Niger saa mbili usiku katika uwanja wa Ibn Batouta nao Mali na Gabon wapimane ubabe saa tano usiku.

Mashindano hayo yatatanguliwa na sherehe za ufunguzi .

Ni mara ya pili kwa Morocco kuwa mwenyeji ya fainali hizo ,baada ya kuyaandaa mwaka 2011.

Mashindano hayo ambayo huandaliwa kila baada ya miaka minne, yanatumika kutafuta waakilishi watatu wa Afrika watakaoshiriki michezo ya Olimpiki mwaka ujao jijini Paris Ufaransa.

Timu nambari nne itacheza mchujo na mpinzani wa Asia kuwani pia tiketi ta kushiriki michezo ya Olimpiki ya mwaka 2024.

Website |  + posts
Share This Article