Kipchoge kuongoza timu ya Kenya ya Marathon ya Olimpiki

Dismas Otuke
1 Min Read

Bingwa mtetezi  Eliud Kipchoge ataongoza kikosi cha wanaume watakaoshiriki marathon ya Olimpiki mwaka huu jijini Paris Ufaransa kati Julai na Agosti mwaka huu.

Kipchoge atalenga kuwa mwanariadha wa kwanza kunyakua dhahabu tatu za Olimpiki mtawalia baada ya kuibuka mshindi mwaka 2016,kabla  ya kuhifadhi taji hiyo mwaka 2020.

Wengine katika kikosi hivho ni bingwa wa Prague marathon mwaja jana Alexander Munyao,Timothy Kiplagat aliyemaliza wa pili katika mbio za Tokyo Marathon mwaka huu,Vincent ngetich aliyemaliza wa pili katika mbio za Berlin Marathon mwaka uliopita na bingwa wa Tokyo marathon Benson Kipruto.

 

Share This Article