Kiongozi wa wengi Nyamira afariki katika ajali

Marion Bosire
1 Min Read

Kiongozi wa walio wengi katika bunge la kaunti ya Nyamira, aliye pia mwakilishi wa wadi ya Nyamaiya Elijah Osiemo Thomas amefariki kwenye ajali ya barabarani iliyotokea karibu na eneo la maai mahiu, barabara kuu ya kutoka Nairobi kuelekea Narok.

Osiemo na wenzake wawili walikuwa wakielekea Nairobi kwa mkutano wa shirika la USAID ajali ilipotokea.

Dereva wa gari lao anasemekana kujaribu kupita pikipiki ambayo ilikuwa imebeba makaa kwa bahati mbaya akagonga gunia hilo, vumbi ya makaa ikasababisha iwe vigumu kwake kuona ndiposa akapoteza mwelekeo na gari likaanguka kwenye mtaro.

Walionusurika walipelekwa kwenye hospitali ya Kijabe kwa matibabu.

Gavana wa Nyamira Amos Nyaribo ametuma ujumbe hospitalini Kijabe kufuatilia hali ya viongozi hao.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *