Kiongozi wa jeshi nchini Gabon apinga uwezekano wa kuandaa uchaguzi mkuu

Dismas Otuke
1 Min Read

Kiongozi wa jeshi nchini Gabon amesema hana haraka ya kuitisha uchaguzi mpya kufuatia kungátuliwa mamlakani kwa Rais Ali Bongo.

Bongo amewekwa kwenye kifungo cha nyumbani tangu aondolewe mamlakani Jumatano wiki hii na kukamilisha utawala wa miaka 56 wa familia hiyo.

Bongo alichaguliwa mwaka 2009,akitwaa mamlaka kutoka kwa marehemu babake aliyeshika madaraka mwaka 1967.

Viongozi wa jeshi walitwaa mamlaka wiki hii na kuamrisha kukamatwa kwa wana wa kiume wa Bongo Noureddin Bongo Valentin, na mawaziri kadhaa kwa ufujaji wa pesa za umma.

Mapinduzi hayo ya Gabon ni hivi karibuni eneo la Afrika magharibi baada ya Guinea, Chad , Niger, Mali na Burkina Faso tangu mwaka 2020.

TAGGED:
Share This Article