Kiongozi wa genge la majambazi akamatwa Nakuru

Tom Mathinji
1 Min Read

Maafisa wa usalama katika kaunti ya Nakuru, wamemtia nguvuni mshukiwa anayedaiwa kuwa kiongozi wa genge la majambazi.

Francis Nderitu Maina mwenye umri wa miaka 21, alikamatwa akiwa kwenye maficho yake katika eneo la Gioto almaarufu London ambalo ni maarufu sana Kwa uhalifu.

Maina anadaiwa kuongoza kundi haramu la Isilando, ambalo limehusishwa na misururu ya visa vya uhalifu katika Kijiji cha Gioto.

Alipotiwa mbaroni, maafisa hao walimpata na kisu ambacho hutumika na wanajeshi, ishara kwamba alikitumia kutekeleza uhalifu.

Baadaye aliwapeleka maafisa hao kwenye maficho yake na kufanikisha kupatikana kwa bunduki bandia.

Kukamatwa kwa mshukiwa huyo ni hatua kubwa katika vita dhidi ya uhalifu katika eneo la Nakuru na kujitolea kwa asasi za usalama kudumisha amani.

TAGGED:
Share This Article