Waziri wa Usalama wa Taifa Kithure Kindiki amesema kuwa wamebaini na hivi karibuni watachapisha majina ya watu wote wanaojihusisha au kuwafadhili majangili sugu katika kaunti ya Lamu.
Waziri Kindiki amekariri kujitolea kwa serikali kutokomeza utovu wa usalama katika kaunti ya Lamu ambao umekuwa ukisababishwa na makundi haramu kama vile Al-Shabaab.
Ameongeza kuwa wale wote watakaokamatwa wataadhibiwa kisheria.