Naibu Rais Kithure Kindiki amewataka Wakenya kujisajili kwa bima ya afya ili kupata mafao.
Kindiki alikuwa akisema haya Jumamosi alipohudhuria kongamano la wahudumu bodaboda katika kaunti ya Embu.
Aidha, Kindiki aliongeza kuwa serikali itaskiza na kuzingatia mapendekezo ya Wakenya jinsi ya kuboresha bima hiyo ya matibabu.
Naibu Rais alisema kuwa takriban Wakenya milioni 18.5 wamejiandikisha kwa bima ya matibabu ya SHA, ikilinganishwa na milioni 9 waliokuwa wanachama wa NHIF.