Kindiki: Ahadi ya Kenya Kwanza kubuni nafasi za ajira inaendelea kutimizwa

Martin Mwanje
1 Min Read
Naibu Rais Prof. Kithure Kindiki akilakiwa KICC na Waziri wa Leba Dkt. Alfred Mutua miongoni mwa maafisa wengine serikalini

Serikali ya Kenya Kwanza inaendelea kubuni nafasi za ajira kama ilivuoahidi wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu wa mwaka 2022. 

Mathalan, katika kipindi cha chini ya miaka miwili iliyopita, Naibu Rais Prof. Kithure Kindiki anasema serikali imewaajiri walimu 76,000 na maelfu ya vijana kuajiriwa katika asasi za usalama.

Kadhalika, Prof. Kindiki anasema vituo 272 vya Habari, Mawasiliano na Teknolojia, ICT vimeanzishwa na hivyo kubuni nafasi za ajira za kidijitali kupitia ubunifu wa maudhui na uendelezaji wa programu mbalimbali.

Naibu Rais anasema lengo la serikali ni hatimaye kubuni vituo 1,450 vya ICT katika kila wadi kote nchini.

Prof. Kindiki aliyasema hayo alipofunga rasmi Maonyesho ya Kitaifa ya Ajira ya Jamhuri katika Jumba la Mikutano ya Kimataifa la Kenyatta, KICC jijini Nairobi.

Kulingana naye, serikali itatumia mbinu tatu kubuni nafasi za aira nchini ikiwa ni pamoja na kile anachosema ni kubuni “Kazi kwa Ground, Kazi Majuu na Kazi Mtandaoni.”

Kenya inakabiliwa na changamoto kubwa ya ukosefu wa ajira na mpango wa serikali ya Kenya kushirikiana na nchi za ughaibuni ili kuhakikisha Wakenya wasiokuwa na ajira wanaondoka nchini kufanya kazi ughaibuni umesababisha vijana wengi kumezea mate kazi za ughaibuni.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *