Naibu Rais Kithure Kindiki amefungua makala ya pili ya mbio za The Great Chepsaita Cross Country, katika kaunti ya Uasin Gishu.
Takriban Washiriki 10,000 walijiandikisha kwa makala ya mwaka huu katika vitengo vya watotot,wazee,vijana chini ya umri wa miaka 20 kilomita 8 wavulana na kilomita 6 wasichana na kilomita 10 wanaume na wanawake.
Mbio hizo ambazo ni za kiwango cha dhahabu, zinatashuhudia washindi wa kilomita 10 wakituzwa shilingi laki tatu nafasi ya pili robo milioni na nambari tatu laki mbili.