Kindiki abuni kamati ya kutekeleza mapendekezo ya Maraga

Dismas Otuke
1 Min Read

Waziri wa usalama wa kitaifa Professa Kithure Kindiki ameteua kamati itakayosimamia utekelezaji wa mapendekezo ya idara ya polisi yaliyopendekezwa na jopokazi la David Maraga.

Kamati hiyo itaongozwa na Katibu wa wizara hiyo Dkt Raymond Omollo.

Wanachama wengine wa tume hiyo ni Makatibu kutoka wizara za Hazina Kuu,urekebishaji wa tabia,utumishi na umma.
Wengine na Kamishna wa Mkuu wa Polisi,idara ya Magereza,tume ya kuratibu mishahara ya wafanyikazi miongoni mwa idara nyinginezo.

Tume hiyo itahudumu kwa kipindi cha miaka mitatu afisini

Share This Article