Professa Abraham Kithure Kindiki ameapishwa rasmi kuwa Naibu Rais wa tatu wa Kenya chini ya katiba mpya iliyorasimishwa mwaka 2010.
Kindiki akiandamana na mkewe Joyce amekamilisha kula viapo viwili akiongozwa na msajili wa idara ya mahakama Winfrida Mokaya.
Kiapo cha kwanza kilikuwa cha uaminifu huku cha ili kikiwa cha utendakazi katika afisi ya Naibu Rais.
Kindiki amekula kiapo saa nne na dakika 53 asubuhi katika ukumbi wa KICC.